Magari Ya Bei Poa Tanzania

Karibuni katika darasa huru na leo tunaelezea  magari ya bei poa yanayopendwa Tanzania. Tutaelezea Magari 6 aina ya Toyota ambayo yanasifika kua na bei rahisi na pia yatakufaa wewe kijana unaetaka kuingia katika ulimwengu wa kumiliki gari. Magari haya ya bei poa yanakufaa kijana mwenye kipato cha kati na chini kwani yana gharama nafuu za uendeshaji na utunzaji.

Kwa Nini Magari Aina Ya Toyota?

Tunaelezea magari ya bei rahisi aina ya Toyota kwasababu spea zake zinapatikana kwa urahisi na kwa bei poa. Kwani kama ndo unaanza kumikliki gari unapaswa kumiliki gari ambayo inatumia mafuta kidogo na pia gharama ya vipuri ni nafuu. Magari haya gharama yake ya ununuzi kuanzia kuagiza nje hadi kufika hapa Dar es salaam Tanzania ni bei nafuu.

1. Aina Ya Kwanza ni Toyota Passo

Magari yaha ni maarufu sana kwa watu hapa Tanzania. Kutoka na kua na bei poa. Magari haya ambayo yana cc 1290 ni magari yanayotumia mafuta kwa uchache sana. Kwa mizunguko ya mjini au kwenda sehemu ambapo sio mbali sana haitakuumiza wewe ambae unaanza maisha. Gharama ya kuagiza Toyota passo ni bei nafuu inaanzia milioni 9 mpaka milioni 12. Inategemea umenunulia Kampuni gani na rate ya Dollar wakati unanunua.

2. Aina Ya Pili Ya Bei Nafuu Ni Toyota Vitz

Magari aina ya Vitz ni magari yenye matoleo mawili. Toleo la kwanza lina cc 990 na toleo la pili lina cc 1290. Hili gari ambalo pia ulaji wake wa mafuta ni mdogo na garama za kununua pia ni za kawaida hivyo kufanya ughrama za undeshaji wa kila siku kua rahisi. Magari haya yana muonekano mzuri na inamfaa mtu yoyote awe mwanamke au mwanaume. Pia unaweza kuyaagiza kwa bei poa kuanzia milioni 9 hadi milioni 14 kutegemeana na Kampuni ya uagizaji, mwaka na ubora wa gari.

3. Aina Ya Tatu Ni Toyota Porte

magari bei rahisi toyota porte

Magari haya huwafaa sana kina mama au kina dada japo kua mwanaume anaweza kuitumia lakini itawafaa Zaidi kina mama. Magari haya yana matoleo mawili, la kwanza cc 1,290 na la pili cc 1,490. Hii ni gari ambayo ina mlango wa umeme kwa hiyo mlango wake unafunguka kwa kurudi nyuma, haifunguki kama milango mingine kwa hiyo kwa mfano akina mama wengi unakuta ni wanene hivyo ataweza kuingia kwa urahisi au kupakia vitu vyake kwa uhuru au kupakia watoto kwenye  gari kwa urahisi. Gari hii imekaaa kikike kike zaidi lakini mtu yoyote anaweza kuimiliki, unaweza kuagiza Porte kwa bei poa kati ya millioni 10 mpaka millioni 13 kutegemeana na Kampuni ya uagizaji

4. Aina Ya Nne Ni Toyota Ractis.

magari bei nafuu ractis Tanzania

Magari haya ni ya kisasa kwa maana kwamba yamekuja na mifumo ya kisasa na ni gari ya miaka ya mbele Zaidi. Kuna Toyota ractis ambazo zinatumia keyless entry kwa maana unaingia bila kutumia funguo, lakini ni gari ambayo ulaji wake wa mafuta ni mdogo hivyo kufanya gharama za uendesha kua rahisi. Gari hii inawafaa wanaume na wanawake. Pia ni gari ambayo katika uagizaji wake bei yake ni rahisi inaanzia milioni 9 mpaka milioni 13. Gari hili lina toleo moja tu ambalo ni injini ya cc 1490. Gari hii inatamfaa mtu yoyote na wala haina shida

5 Aina Ya Tano Ya Bei Poa Ni Toyota Runx

Toyota Runx ni magari mazuri sana na yanawafaa wakaka na pia  wamama, ni gari ambayo mtu yoyote haimkatai. Ni gari ya chini lakini ni gari ambayo ukitaka kuibadilisha kwa kuiboresha kua na muonekano mzuri zaidi ni rahisi na hupendeza sana.  Gari hii ina matoleo wawili, la kwanza  lina cc 1,490 na toleo lingine lina cc 1,790. Hii ya cc 1,490 ulaji wake wa mafuta ni wa kawaida. Hii ya cc 1,790 ulaji wake wa mafuta ni wajuu kidogo kulinganisha na toleo la 1,490 Lakini ni gari ambayo inakufaa wewe ambaye unataka kuanza maisha ya kumiliki gari. Bei ya kuagiza Toyota Runx inaanzia milioni 12 mpaka milioni 14 kutegemeana unaagiza kupitia Kampuni gani ya kuagiza magari Tanzania

magari bei poa Toyota ist

Toyota IST ni gari namba moja kwa uuzwaji hapa nchini Tanzania, yaani number one selling car. Hii ni gari ambayo haimkatai mwanaume na haimkatai mwanamke. Tumekwisha fanya review ya Toyota ist unaweza kuipitia hapa. Ni gari ambayo ina matoleo mawili, la kwanza ni cc 1,290 na la pili 1,490. Uzuri wa gari hii matoleo yote mawili hayali mafuta na pia upatikanaji wa vipuri vyake ni rahisi nn kwa bei poa kote Tanzania

Pia Soma Mada Hizi Pendwa

0

Magari Yenye Punguzo

Tutakutumia Moja Kwa Moja Kwenye E-Mail Yako. Hii Sio Ya Kukosa!

(Strictly No Spam)